After Yamaha launching the MT-09 Tracer, a touring version of the street bike MT-09 (FZ-09 in the US), Yamaha is now planning to apply the same… Visit the link above to read the full story.

[via MotorCycleFeed.com – Must-Read global Motorcycle News site]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }

Dar es Salaam. Nyumba ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Mwalimu Julius Nyerere, Paul Sozigwa imeuzwa katika mazingira ya kutatanisha na mke wake Monica Kuga baada ya mwanahabari huyo kupata maradhi ya kupoteza kumbukumbu. Kuga aliiuza  nyumba hiyo kwa Mahamood Duale kwa Sh600 milioni mwaka 2010, huku watoto wake wanne wa Sozigwa wakipinga uuzwaji huo wakidai kuwa baba yao aliwakabidhi nyumba hiyo mwaka 1998. Mtoto wa mwisho wa Sozigwa ambaye pia ametajwa kama msimamizi wa mirathi, Moses alisema wana vielelezo vya wosia aliowaachia baba yao akiwa Finland kabla ya tatizo lake la kupoteza kumbukumbu halijawa kubwa. “Tulirekodi kila kitu na ushahidi wa maandishi upo, baba alisema nyumba ile ni ya watoto na siyo yake wala ya mke wake. Lakini pia tulirekodi sauti yake, tunashangaa kwanini mama ameiuza,” alisema Moses. Kwa maelezo ya wanafamilia hao, Kuga aliachana na Sozigwa mwaka 1974 na kufungua kesi ya kudai talaka mahakamani jambo ambalo baba yao alilipinga. “Alitaka kuachana na baba tena sisi tukiwa wadogo ili wagawane mali, lakini baba hakukubali, tunashangaa iweje leo arudiane naye halafu auze nyumba?” alihoji Moses. Moses alieleza kuwa mama yao alimchukua Sozigwa na kuishi naye kama kisingizio cha kujihalalishia  uuzwaji wa nyumba hiyo iliyopo maeneo ya Kurasini, karibu na shule ya Sekondari ya Jitegemee. “Mama alimkana baba na wameachana kwa miaka zaidi ya 34 na aliidai talaka hadi mahakamani kwa nguvu, halafu baba alipoanza kuumwa anadai anataka kumlea kumbe ni ujanja wake  tu, alitaka kuuza eneo la familia,” alidai mtoto huyo. Kwa mujibu wa wanafamilia hao, Kuga alighushi hati ya nyumba hiyo na kuiuza kwa Duale lakini baadaye aliwataka wampe hati halisi ili amkabidhi Duale. Lakini baada ya kuona kuwa hawezi kuipata, kwa kushirikiana na Duale walianza kumsumbua Moses na hatimaye walimfungulia kesi mahakamani. Hata hivyo, baada ya Duale kuzungumza na wakili wa familia ya Sozigwa, aliambiwa ukweli kuwa hiyo nyumba ina utata wa wanafamilia hali iliyomsababishia Duale mshtuko hadi kupooza. “Huyu Duale alizungumza na wakili wetu, akaambiwa ukweli kuwa asinunue hiyo nyumba kwa kuwa haina hati na alipoonyeshwa hati halisi alishtuka na kupata kiharusi kwa sababu alikuwa ameshalipa fedha zote,” alisema Moses. Akiendelea kusimulia, Moses alisema mauzo ya nyumba hiyo yana utata na kuna dalili ya rushwa kwani yameidhinishwa na baraza la ardhi la Wilaya ya Temeke ambalo kwa kawaida, lina haki ya kuidhinisha mauzo ya nyumba yenye thamani ya Sh50 milioni na chini ya hapo, wakati thamani halisi ya nyumba hiyo ni Sh900 milioni. “Tunashangazwa na kitendo cha mama kuuza nyumba hiyo kwa Sh600 milioni wakati tathmini iliyofanywa mwaka 2010 ilionyesha kuwa ina thamani ya Sh900 milioni,” alisema Moses. Moses ambaye alizungumza kwa niaba ya ndugu zake watatu, Salome, Irene na Ephata alisema licha ya mama yao kuuza nyumba kwa mamilioni ya fedha lakini alikataa kusaidia kutoa fedha za kumpeleka baba yao nchini Finland kwa matibabu. “Ilitubidi kutembeza bakuli hadi kwa Rais Jakaya Kikwete ili tupate msaada wa matibabu ya mzee,” alisema. Mwananchi lilizungumza na Kuga ambaye alisema anawashangaa watoto wake kwa kushindwa kujua sheria zinavyofanya kazi na kuanza kumrushia tuhuma zisizo na ukweli kuwa ameuza nyumba kwa ujanja. “Hii kesi imeenda mahakamani  hadi mahakama kuu na nimeshinda mara tatu, lakini hawa wanaona kuwa wao ndiyo wana haki ya nyumba ambayo mimi na baba yao tuliijenga, wanakata rufaa kila siku,” alisema. Alieleza pia sababu za kuishi na Sozigwa licha ya kuwa walitengana kwa zaidi ya miaka 34. Alisema baada ya kuona hali ya mumewe huyo siyo ya kuridhisha aliamua kurejea kumtunza na siyo kwa ajili ya nyumba. “Nilimhurumia mzee nikaamua kuishi naye ili nimlee na ndiyo hapo tulipokubaliana naye tuiuze nyumba,” alisema. Kuga ambaye aliwahi kugombea ubunge wa Temeke kwa tiketi ya DP mwaka 1995, alisema watoto wake hao walifikia hatua ya kuficha hati halisi ya nyumba hiyo ili kuzuia uuzwaji. Lakini hata hivyo, Kuga alisema yeye na wakili wake walitoa matangazo kwenye magazeti kuwa hati hiyo imepotea ili kupata kibali kutengeneza hati mpya ili waweze kuiuza nyumba hiyo. “Hali ya baba yao ni mbaya lakini naona na hawa watoto hali yao ni mbaya zaidi kwa sababu hawajui kitu wanachokifanya; nyumba ni yetu mimi na mzee wao kinawauma nini? Alihoji. Kadhalika Kuga alisema mpaka sasa Duale tayari ana hati na ameshakuwa mmiliki kamili wa nyumba hiyo. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }

Dar es salaam. Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ameishukia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushindwa kutangaza mgawanyo wa majimbo, akisema kuchelewa huko kunavuruga mipango yao. Ukawa, inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, imekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia ngazi ya urais hadi diwani na viongozi wa vyama hivyo wameshakutana mara kadhaa kuzungumzia kugawana majimbo kulingana na nguvu ya chama kwenye eneo husika. Hata hivyo, vimeshindwa kumalizia kazi hiyo kutokana na kutokamilika kwa mgawanyo wa majimbo kama NEC ilivyoahidi Mei 12 kuwa majimbo mapya kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 yangetangazwa Juni 30. Akizungumza jana, Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema aliitupia lawama NEC akisema wakati huu ilitakiwa kuwa imeshamaliza suala la majimbo na kushughulikia mambo mengine. “Tunataka kutengeneza ratiba ya mpango kazi, lakini tunashindwa. Tunataka tujue majimbo mapya ili twende huko, lakini sasa tunashindwa na muda unakwenda,” alisema Mbowe. Akizungumzia ukimya wa kutangaza majimbo hayo licha ya kusema ingefanya hivyo Juni mwishoni, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema hadi sasa Tume hiyo haijakamilisha ugawaji wa majimbo lakini bado wanaendelea na mchakato huo. Alisema Tume yake imeamua kugawa majimbo hayo kwa kuzingatia vigezo mbalimbali, ikiwamo idadi ya watu, upatikanaji  wa mawasiliano, hali ya kijiografia na kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge za mwaka 2010. Jaji Lubuva pia alisema Tume itayagawa majimbo hayo kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu bora, hali ya kiuchumi kwa kuweka uwiano kati ya eneo moja na jingine, mawasiliano ya simu na vyombo vya habari kwa ajili ya kupata mwakilishi atakayeharakisha maendeleo katika eneo husika. Wakati ikisuasua kutangaza majimbo mapya ya uchaguzi, NEC pia inakabiliwa na kibarua kingine cha kumalizia uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura. Kazi hiyo imekumbwa na matatizo kadhaa na inatakiwa ikamilishwe katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, lakini imeahirishwa kutokana na kuchelewa kwa mashine zinazotumika za teknolojia ya mfumo wa kuchukua alama na taswira za mpigakura (Biometric Voters Registration). Jaji Lubuva alisema kuwa kuna baadhi ya majimbo ambayo ni makubwa, jambo ambalo alisema linatokana na ongezeko la watu nchini. Ugawaji wa majimbo unatakiwa kufanyika mara kwa mara au angalau mara moja baada ya miaka 10. “Ugawaji wa majimbo ulifanyika kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kwa kuwa sasa tunaelekea uchaguzi mwingine, lazima tufanye hivyo,” alisema  Jaji Lubuva. Kauli ya Mbowe Akizungumzia kusuasua huko kwa ugawaji majimbo, Mbowe alisema NEC inataka ifanye mambo mengi kwa wakati mmoja. “Tume imezidiwa na majukumu; inataka kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, huku muda ukiwa haupo. Kila siku wanaahirisha hili mara lile na mengine hawayatolei taarifa,” alisema Mbowe. Alisema tangu Tume hiyo ilipotangaza kugawa majimbo ya uchaguzi nchi nzima, bado mpaka leo haijafanikisha shughuli hiyo, jambo ambalo linasababisha kuchelewa kwa umoja huo kugawana majimbo. “Uchaguzi ni vita,” alisema Mbowe. “Sasa sijui wanasubiri nini? Mpaka leo hawataki kutangaza hayo majimbo waliyosema wanayagawa, sisi tunasubiri wakimaliza tu tunaanza mchakato wa kugawana ila kwa hali ilivyo sasa, hatuwezi kufanya lolote.” FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }

MKAZI wa kijiji cha Igongwa wilayani Maswa mkoani Simiyu, Majingwa Ndushi (32) amekamatwa na jeshi la Polisi baada ya kutoroka akikwepa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kumuua baba yake mzazi, Ndushi Majingwa (65) kwa kumkata na shoka kichwani.   Mbele ya mahakama hiyo, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa jeshi hilo, Mkaguzi wa polisi Nassibu Swedy, kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo, Mei 30 mwaka huu, saa tatu asubuhi kijijini hapo.   Alidai kuwa, kabla ya kufanya mauaji hayo mshtakiwa huyo alifika nyumbani kwa baba yake akiwa na shoka mkononi na kumkuta akiwa amekaa kwenye kiti na kisha kuanza kulumbana kwa maneno na hivyo kushindwa kuelewana, ndipo alipomshambulia kwa kumkata kwa shoka kichwani na kufa papo hapo.   Swedy alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Tumain Marwa, kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kati ya marehemu na mwanae huyo.   Alisema mara baada ya kufanya tukio hilo alitoroka lakini baada ya muda mfupi, alikamatwa na kisha kufikishwa katika kituo cha polisi cha wilaya ya Maswa.   Hata hivyo, mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo, haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji na hivyo kesi hiyo itatajwa tena Julai 15, mwaka huu, na mshitakiwa amepelekwa rumande. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana imeshindwa kumsomea maelezo ya awali Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya matusi na kushindwa kuhifadhi silaha.   Kesi hiyo ilitajwa jana kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali lakini iliahirishwa kwa kuwa Hakimu Mkazi Wilfred Dyansobera anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo mahakamani.   Hakimu Mkazi, Thomas Simba aliahirisha kesi hiyo hiyo Julai 20, mwaka huu kwa ajili ya washitakiwa hao kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Dyansobera.   Mbali na Gwajima washitakiwa wengine, ni Mlinzi wake, George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze (39) na Mchungaji Georgey Milulu (31) wanakabiliwa na shitaka la kukutwa na silaha pamoja na risasi kinyume cha sheria.    Katika kesi ya kwanza namba 85, Gwajima anadaiwa kati ya Machi16 na 25, mwaka huu katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam alitoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu wa Kanisa Katoliki Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akimueleza Askofu kwamba ni mtoto, mpuuzi asiye na akili katika namna ya kwamba ingeleta uvunjifu wa amani.    Katika kesi nyingine namba 84 , Gwajima anakabiliwa na mashitaka ya kushindwa kuhifadhi silaha na risasi jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya uhifadhi wa silaha za moto.    Anadaiwa kati ya Machi 27 na 29, mwaka huu, ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam, alishindwa kuhifadhi silaha aina ya Beretta namba CAT 5802, risasi 3 za pisto na risasi 17 za shotgun.    Katika mashitaka mengine yanayowakabili washitakiwa wengine, inadaiwa Machi 29, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ Mikocheni ‘A’ walikutwa wakimiliki silaha na risasi hizo bila ruhusa kutoka mamlaka husika. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }

WATU watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti katika Wilaya za Tarime na Rorya akiwemo mtu aliyeuawa wakati wanagombania mwanamke.   Waliokufa ni Chacha Mwita (24) aliyechomwa kisu kifuani na mwenzake wakigombea mwanamke wa baa huko Sirari.    Wengine ni Juma Nguka (25) aliyeuawa na watu wenye hasira baada ya kutuhumiwa kupora pikipiki yenye namba za usajili MC 936 ACA, mali ya Erick Jumanne mkazi wa Kijiji cha Mkoma.   Tukio lingine ni kufa maji kwa mvuvi aliyefahamika kwa jina la Wambura Maregeri (30) mkazi wa kijiji cha Muhundwe aliyekufa maji baada ya Boya kutoboka.   Kaimu Kamanda wa Polisi Tarime Rorya ACP Swetbert Njewike alisema kuwa matukio hayo matatu ya vifo yalitokea Julai mosi mwaka huu katika Wilaya za Rorya na Tarime.   Akielezea tukio la baa ambalo Mwita aliuawa, alisema siku hiyo marehemu akiwa baa moja katika mji wa Sirari, Tarime, nyakati za saa moja jioni kulitokea ugomvi kati ya marehemu na mtu mwingine ambaye hajafahamika jina lake wakigombania mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Dina.   Alisema wakati wa ugomvi huo, Mwita alichomwa kisu kifuani na aliyefanya kitendo hicho alitoroka ambapo majeruhi huyo alitokwa damu nyingi na alipofikishwa Hospitali ya Wilaya Tarime alifariki dunia.   Alisema Nguka yeye alipoteza maisha baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa kuiba pikipiki.    Akasema Maregesi alikufa maji baada ya boya lililotengenezwa kienyeji alilokuwa anatumia katika uvuvi kutoboka na kuzama majini hali iliyopelekea kifo chake.   “Jeshi la Polisi linafanya msako wa watuhumiwa wa mauaji Chacha Mwita na watuhumiwa waliohusika katika mauaji ya Nguka ili waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria,” alisema.   Aliwaonya wananchi kutojichukulia sheria mikononi ya kuwauawa watu wengine badala yake wawafikishe katika vyombo husika vikiwemo vya Dola.     Aliwaomba raia wema kutoa taarifa mara watakapowaona watuhumiwa hao wa mauaji hayo ii wakamatwe. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }

Afande Sele amesema akiingia bungeni hawezi kuwasahau wasanii wenzake kama walivyosahauliwa na wasanii wabunge waliotangulia kuingia mjengoni. Rapper huyo  atawania kiti cha ubunge wa jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi cha ya chama cha ACT na amesemakuwa akiingia bungeni wasanii watarajie mambo makubwa kutoka kwake.   “Lengo langu kubwa kwa wasanii ni kupigania haki za wasanii,” Amesema  Afande Sele   “Nimegundua tukizungumzia haki za wasanii kwenye muziki kwa kuimba tu, hakuna kitachofanyika. Viongozi hawana shinikizo la kutekeleza, wanazungumzia tu kidogo halafu wanaacha.    “Lakini nimeona ukiingia bungeni wasanii tutashiriki moja kwa moja kwenye utungaji sheria za nchi.    “Suala la haki za wasanii nitakuwa niko nalo karibu sana na nitalipigania kwa namna yoyote kwa sababu nipo kwenye chombo cha maamuzi na nina rungu mkononi,” ameongeza msanii huyo.   “Lakini leo hii hata nikiwa nazungumza sina silaha yoyote, lakini tukiingia bungeni tunaweza kupaza sauti na zikasikika kwa sababu tupo kwenye chombo cha sheria na kina mamlaka na uwezo.    “Unajua kila anayeingia bungeni unakuta baadaye anabadilika, mimi nina upeo mkubwa tofauti na wabunge wanaomaliza muda wao. Inaonyesha waliingia kwenye siasa kwaajili ya kutafuta maslahi. Kwahiyo wasanii watarajie kuona sheria za haki miliki zikipatikana au zile zilizopo zikifanyiwa marekebisho,” amesisitiza.   “Kwa sasa hivi bungeni hakuna mtu mwenye uchungu na sanaa, wasanii ambao walibahatika kuwa wabunge wameingia bungeni nao wamegeuka mafisadi vilevile.   “Wamekuwa wawekezaji wa biashara, wamedharau shida za wasanii. KwaHiyo mimi nafikiri bungeni kulikuwa hakuna wasanii ambao wanatuwakilisha, wasanii tunaotaka kuingia bungeni sasa hivi tuna wito. Kwahiyo watu wategemee kuona mabadiliko makubwa sana kwenye sanaa.”   Katika hatua nyingine, Afande amesema kwa sasa hatoweza kutoa wimbo wowote mpaka uchaguzi utakapopita.   “Ningependa sana mashabiki wa muziki wangu wasubiri uchaguzi upite ndio wasikie kazi mpya kwa sababu tayari akili na mawazo na malengo yangu yapo kwenye uchaguzi. Mimi nimeona nisiwa-disturb kwa kitu chochote mpaka uchaguzi upite.    “Kwa sababu hili ni jambo muhimu sana linatokea kwenye taifa na ni maisha yao. Kwahiyo watu wajitokeze kujiandikisha pamoja na kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka.” FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }

Bado una wasiwasi juu ya maelewano kati ya muimbaji wa Nigeria, Davido na Diamond? Pamoja na Diamond kujibu kwenye Interview mbalimbali kuwa hawana tatizo, Davido naye ametoa uthibitisho mwingine kuwa hakuna ‘beef’ kati yao. Ni jambo gumu kupost kitu kinachomhusu mtu ambaye hamna maelewano, ndio maana kwa post hii ya Davido watu wanapaswa kufahamu kuwa jamaa hawa wawili wanaiva chungu kimoja, na tutarajie kuwaona wakitumbuiza tena pamoja kwenye tuzo za MTV mwezi huu.   Baada ya MTV kutaja majina ya wasanii wa Afrika watakaotumbuiza wakati wa utolewaji wa tuzo za MAMA akiwemo Davido na Diamond, Davido alipost picha ya performance aliyofanya na Diamond mwaka jana kwenye tuzo hizo. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }

Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni amewekwa chini na familia yake na kupewa onyo kuhusu wanaume pamoja na maadili.   Kwa mujibu wa chanzo, Rose aliambiwa maneno mengi na familia yake ikimtaka ajirekebishe na haswa ajitume zaidi katika kazi zake anazofanya.   “Familia yake imeamua kumuweka chini na kumwambia mengi kuhusu maisha haswa ikimtaka ajirekebishe tabia yake kwa ujumla,” kilisema chanzo.   Rose alipotafutwa kuweka wazi juu ya hili, alifunguka; “Kila familia ina utaratibu wake, kwahiyo mimi kuwekwa na familia na kupewa onyo wala siyo suala la ajabu.” FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }

Nchi ya Msumbiji imepitisha sheria inayohalalisha mapenzi ya jinsia moja, na kuwa miongoni mwa nchi chache Barani Afrika zinazoruhusu mapenzi ya jinsia moja.   Sheria hiyo iliyowekwa na wakoloni wa nchi hiyo, Ureno awali ilifutwa na Bunge la nchi. Watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja, wametaja hatua hiyo kama ushindi mkubwa.   Hata hivyo nchi nyingi za Afrika zimeweka sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja. Nigeria ilipiga marufuku na kuweka adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wakati huo Uganda nayo imeapa kurejesha sheria kali kuharamisha mapenzi ya jinsia moja. Sheria ya awali ilitupiliwa nje na mahakama ya kikatiba.   Msumbiji sasa anajiunga na mataifa mengine ikiwa ni pamoja na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ivory Coast na Afrika Kusini ambapo siyo hatia kuwa mpenzi wa jinsia moja. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

{ 0 comments }